Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir amewahimiza wakazi wa Mvita na Pwani kwa jumla kujiandikisha kwa wingi kama wapiga kura pale tu tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini itakapoanza usajili.

Akizungumza eneo la Jua Kali wadi ya Tudor siku ya Jumapili, Abdulswamad alieleza kuwa ni haki ya kikatiba kwa wananchi kujiandikisha na kumiliki kadi za kura kama silaha mwafaka ya kubadilisha uongozi.

Aliwasihi vijana kuwachaguwa viongozi wenye maoni na nia ya maendeleo yatakayo wafaidi wananchi.

Aidha, aliwasisitiza vijana kuchukua vitambulisho ili kuwa raisi kwao kujiandikisha kama wapiga kura.

Hatua hii inajiri baada ya IEBC kutarajiwa kuanza zoezi la usajili wa wapiga kura hivi karibuni.