Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Nakuru Mary Mbugua amewashauri akina mama kuhakikisha wanavalia mavazi nadhifu ya ndani kila wakati.

Akizungumza na akina mama wa kanisa katoliki, Catholic Women Association ( CWA) Jumamosi, Mbugua alisema baadhi ya wanawake huvaa chupi chafu zenye aibu na hivyo wakijipata kwenye ajali wanabakia na fedheha chungu nzima.

"Unajua watu wengine wanavaa tu nguo ovyo ovyo na unajua unaweza kufika kwa barabara matatu ianguke. Inapoanguka, watu watalazimika kukubeba hadi kwenye hospitali lakini unapovuliwa nguo, hapo aibu unaipata," Mbugua alisema.

Mbugua pia aliwashauri akina mama wote kuhakikisha wanatunza vitanda kwenye ndoa zao ipasavyo sawa na kuwajali waume wao.

"Mume wako anapotoka nyumbani, hakikisha umeangalia yale mavazi ambayo amevaa," Mbugua alisema.

Wakati huo huo, aliwahimiza wanawake kutatua mizozo yao ya nyumbani badala ya kukimbilia viongozi kama vile chifu.