Aliyekuwa mbunge wa eneo bunge la Kitutu Masaba Walter Nyambati ametuma risala za rambi rambi kuiliwaza familia ya mwendazake bwana Kamonde aliyeuliwa na wahuni.
Ujumbe uliochapishwa mtandaonni, mbunge huyo wa zamani ameonyesha kusikitishwa na mauaji hayo na ameihadi familia ya mwendazake na kuahidi kusimama nao katika maombi na anapania kuwatembelea ili kuwafariji zaidi.
"Ninaomboleza na familia ya bwana Kamonde. Nitasimama nao kwa maombi na nina mipango kuwatembelea ili kupeana usaidizi wangu wa dhati," ulisoma sehemu ya ujumbe.
Aidha, Nyambati amesema hajafurahishwa na hali ya ukosefu wa usalama katika kaunti ya Nyamira hasa wadi ya Bokeira iliyo eneo bunge la North Mugirango.
"Nimehuzunishwa mno na viwango vya usalama katika kaunti ya Nyamira, hasa wadi ya Bokeira ambapo kumekuwa na mauaji hivi karibuni," ulisoma ujumbe.
Aliendelea kusema kuwa mauaji hayo yaliyofanywa na genge lisilojulikana la wahuni, inafaa kulaaniwa kwa maneno yenye nguvu huku akiongezea kuwa usalama unapaswa kuwa hakikisho la serikali kwa wananchi sambamba na kuheshimu haki zao.
"Mauaji haya yaliyotendwa na kundi la majambazi yanafaa kulaaniwa sana. Usalama pia unafaa kuwa hakikisho kubwa la serikali kwa wananchi na kuheshimu haki za binadamu," ulisoma huo ujumbe.