Seneta mteule Emma Mbura amesema kuwa mrengo wa Jubilii umeanzisha mikakati ya kutambua mgombea wa kiti cha ugavana katika Kaunti ya Mombasa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Bi Mbura amesema kuwa mazungumzo kati ya viongozi na wafuasi yatakuwa nguzo muhimu kuhakikisha wanachagua mgombea atakaye chuana na Gavana wa Mombasa Hassan Joho, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

Katika kikao na wanahabri jijini Mombasa, seneta huyo amesema kuwa atahakikisha kuwa Jubilee wanaibuka na ushindi katika kinyanganyiro hicho.

“Kuna ushindani mkali kutokana na idadi ya wagombea wanaonuia kusimama na chama cha Jubilee kutetea kiti cha ugavana, lakini wajumbe wa chama ndio wataamua nani atasimama,” alisema Mbura.

“Hatutaki watu wa Nairobi waseme Babangida tosha, Shahbal tosha au Mwaboza tosha. Hapo kutakua hakuna demokrasia. Watu wa Mombasa wanajua ni gavana yupi wanataka kupitia tiketi ya jubilee,” aliongeza.

Aidha, ameongeza kuwa idadi kubwa ya wagombea wanaojitokeza kujiunga na chama cha JAP ni dalili tosha kuwa chama hicho kitaimarika mashani licha ya kutozinduliwa rasmi.

Mbura pia amependekeza wajumbe kupewa nafasi ya kuwachagua wagombea katika misingi ya demokrasia, ili kuepuka kushuhudiwa kwa ati ati kati ya wafuasi wa chama hicho.

Aidha, amesema kuwa amefurahishwa na idadi kubwa ya wanasiasa wanaohamia Jubilee kutoka mrengo wa upinzani.