Serikali ya kaunti ya Kisii imehimizwa kukamilisha miradi iliyoanzisha katika wadi ya Magenche eneo bunge la Bomachoge Borabu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wito huo umetolewa baada ya kuofiwa kuwa huenda miradi hiyo haitokamilika baada ya kuchukua mda mrefu na kukwama huku serikali hiyo ikiombwa kujaribu kuikamilisha ili kuleta usawa kama ilivyo katika wadi zingine.

Akizungumza siku ya Jumatano mjini Kisii, Mwakilishi wa wadi ya Magenche Timothy Ogugu alisema baadhi ya miradi ambayo serikali ilianzisha kwa wadi yake na haijakamilika.

Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na ukarabati wa barabara, miradi ya maji, ukarabati wa viwanja na ujenzi wa madarasa ya chekechea.

“Si vizuri miradi ya maendeleo kuanzishwa na kutokamilika katika wadi yangu naiomba serikali ya kaunti ya Kisii kujaribu kuimaliza miradi hiyo ili tuanze mengine tofauti tunapoendelea kusonga mbele,” alisema Ogugu.