Mwakilishi wa wadi ya Kisii ya kati Wilfred Monyenye amelalamikia kutofikishwa mahakamani kwa washukiwa watatu waliodaiwa kumchoma mkaazi mmoja mishale sita siku ya Jumamosi katika uwanja wa Erera mjini Kisii .

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kulingana na Monyenye ni heri haki itendeke kwa wote kwani mkaazi huyo aliyedungwa mishale hakuwa na makosa ila alipokuwa anapita katika uwanja huo alidungwa mishale huku ikibainika kuwa washukiwa hao bado hawajafikishwa mahakamani.

Akizungumza katika bunge la kaunti ya Kisii Monyenye alisema wakaazi wako huru kupita katika uwanja wa Erera hadi njia tofauti ipatikane ambapo wakaazi watakuwa wanapitia.

“Tangu siku ya Jumamosi washukiwa hao hawajafikishwa mahakani kusomewa mashtaka waliyoyafanya kwa kudunga mtu mishale,” alisema Monyenye.

“Spika naomba ukweli na haki itendeke kwa wakaazi wa kaunti yetu ya Kisii,” aliongeza Monyenye.

Aidha, spika wa bunge hilo Okerosi Ondieki aliomba kamati ya bunge kuhusu sheria kuchunguza madai hayo na kurudisha ripoti kwa bunge hilo ndani ya siku tano.