Waathiriwa wa mkasa wa moto Michatha Molo wamepokea msaada hii leo baada ya nyumba zao kuteketezwa. Waathiriwa hao walipokea msaada huo kutoka kwa MCA wa eneo hilo Michael Wang’ombe na kikosi cha msalaba mwekundu.

Share news tips with us here at Hivisasa

“Tunashukuru sana kwa msaada huu na tungeomba yeyote anataka kutusaidia afanye hivyo,” Jane Wambui alisema.

Wang’ombe alisema mkasa huo uliathiri familia takriban 38.

“Familia hizi zimeathirika sana. Kama watu wako na uwezo wajitokeze na kuwasaidia,” Wang’ombe alisema.

Familia hizo zilipoteza kila kitu kwenye moto huo ulioteketeza nyumba zao Jumanne alasiri.