Waimbaji katika kanisa zote ambazo zinahitaji kutoa kanda za nyimbo katika wadi ya Sensi eneo bunge la Kitutu Chache Kaskazini kaunti ya Kisii wana kila sababu ya kutabasamu. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya Mwakilishi wadi hiyo Onchong’a Nyagaka kutangaza kuwa atagharamia pesa zinazo itajika kunakili mianda hiyo.

Mwakilishi huyo alisema waimbaji wengi katika makanisa mbalimbali ya wadi yake hawasambazi injili inavyostahili kupitia kanda za nyimbo kufuatia ukosefu wa hela na sasa ameweka bayana kuwa atagharamia shughli hiyo ili injili ipenye kote katika wadi yake.

“Kuna waimbaji wa kanisa ambao wako na nyimbo nzuri lakini hawana uwezo wa kurekodi na kutengeneza kanda hizo, mimi kama kiongozi wa Sensi nitagharamia pesa zote wanazohitaji ili kutoa nyimbo hizo katika ukanda,” alisema Nyagaka.

Wakati huo huo, Nyagaka aliomba viongozi wa kanisa zote zile zinazohitaji kurekodi nyimbo zipate kumjulisha ili aweze kugharamia.