Wakulima kutoka wadi ya Kabazi iliyoka ndani ya kaunti ndogo ya Subukia wameirai serikali ya jimbo ya Nakuru kujenga kampuni ya avokado katika eneo hilo ili kuwakomboa kutoka mikononi mwa madalali.
Wakizungumza katika shamba la Jumatatu hii leo wakati wa zoezi la kupata miche ya zao hilo kutoka kwa serikali ya kaunti yya Nakuru, wakulima hao wamesema tunda hilo linafanya vyema katika maeneo hayo japo mawakala huwanunulia mazao yao kwa bei ya chini mno ikilinganishwa na faida yao.
Wakiongozwa na Mkulima Joseph Kangethe, wakulima hao wamesema madalali hununua tunda hilo kwa kati ya shingi 3 na shilingi tano huku wakiuza kwa shilingi 10 hadi 20.
Wameirai serikali ya kaunti kuunda kiwanda hicho karibu na wakulima kwani kitakuwa cha manufaa kwao na kwa maeneo yote kwa jumla katika kaunti ya Nakuru.
Kaunti ya Nakuru imekuwa ikiwarai wakaazi wa eneo hilo la kabazi kugeuza ukulima wao kando na mahindi na maharage huku ikiwapa miche na mbegu ya mimea kama Pareto, Kahawa na Avocado kupitia kwa mwakilishi wadi Mwangi Waithaka.
MCA waithaka, amewahakikishia wakulima kwamba kaunti ya Nakuru itazidi kujali masilahi yao ili kuzalisha kiwango cha juu cha chakula katika maeneo yote.
Ametaja kando na kuweko na kiwanda cha tunda hilo, kuna haja ya kuwanza na muungano wa wakulima wa zao hilo ambalo kutachangia kuuza matunda yao kupitia kwa vyama vya ushirika ili kutatua shida zao.
Amesema kwa kufanya hivyo mawakala watakosa nafasi ya kununua mazao yao huku wakulima wakinufaika kwa kuuza mazao yao moja kwa moja.