Mwakilishi wadi ya Kivumbini Vitallis Okello maarufu Major ametoa wito kwa wakaazi kutumia vyema vyoo walivyojengewa kwa ushirikiano na afisi yake.
Akizungumza mapema Jumamosi wakati wa kuangazia hali ya vyoo hivyo katika eneo la Kivumbini 4, mwakilishi huyo alisema kuwa iligharimu fedha kujenga na kukarabati vyoo hivyo.
"Vyoo hivi ni muhimu sana katika kuhakikisha usafi wenu na afya, na mwafaa kuvitumia vyema," Okello alisema.
Wakati huo huo aliwahakikishia wakaazi kwamba swala la taa za barabarani na mitaani zitawekwa ili kuimarisha usalama katika wadi hiyo.