Mwakilishi wadi ya Elburgon Nakuru Florence Wambui ameshtumu vikali baadhi ya wanasiasa wanaokosoa ziara ya Rais Uhuru Kenyatta maajuzi katika kaunti ya Nakuru. Katika mahojiano Kwa njia ya simu MCA Florence alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba kuna baadhi ya viongozi wasioona maendeleo yanayoshuhudiwa.

Share news tips with us here at Hivisasa

"Tunajua kuna watu ambao kazi yao ni kukosoa hata pasipostahili kukosolewa," Wambui alisema.

Wakati huo huo alitoa wito kwa wakaazi wa Elburgon kuepuka wanasiasa potovu na badala yake washirikiane na uongozi uliopo kwa sasa. Anasema kuwa ni jambo la busara Kwa viongozi waliochaguliwa kuheshimiwa.