Mwakilishi wa wadi ya Nessuit eneo bunge la Njoro ambapo shamba tata la Ngongongeri linapatikana ametaka uchunguzi ufanywe kuhusu mauaji ya mkaazi mmoja kwenye shamba hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

MCA Samwel Tonui Jumatatu alisema haki inafaa kutendekea kwenye utata unaozunguka shamba hilo.

Tonui alisema alikuwa amekutana na mkaazi Stephen Munyereria kabla ya kuuawa kwa kupigwa riasai. Tonui alisema ni sharti sharia ifuatwe katika kutatua mzozo huo.

“Tulikuwa nay eye mchana na akasema atafikiria kuhama hapa kwani anahofia maisha yake kutokana na mzozo huu,” Tonui alisema. Munyereria inadaiwa aliuawa na mmiliki mmoja wa shamba kwenye eneo hilo baada ya ugomvi kati yawawili hao.

Taharuki ilitanda kwenye eneo hilo Jumapili na Jumatatu huku polisi zaidi wakitumwa kushika doria.