Spika wa bunge la kaunti ya Kisii Okerosi Ondieki amesema wawakilishi wadi watano katika kaunti hiyo wameelekea mahakamani kuzuia Tume ya Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutoandaa uchaguzi mwezi wa nane mwaka ujao.
Ondieki alisema kuwa kile kiliwafanya wawakilishi hao kuelekea mahakamani ni kuwa katiba inaeleza kuwa wanastahili kuwa afisini miaka mitano na kusema ikiwa uchaguzi huo utafanyika mwezi wa nane basi watakuwa afisini miaka minne tu na hivyo watakuwa wamekiuka katiba.
“Wawakilishi watano wa kaunti yetu ya Kisii na watatu kutoka kaunti ya Homabay walienda mahakamani kushitaki tume ya IEBC kutofanya uchaguzi mwezi wa nane mwaka ujao ili waweze kumaliza wakati wao wa miaka mitano afisini jinsi ilivyokatibiwa kikatiba,” alisema ondieki.
Aidha , Ondieki alisema kesi hiyo itasikizwa 5/4/2015.