Meli ya watalii.[mediamaxnetwork.co.ke]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Sekta ya utalii nchini inazidi kuimarika huku meli zaidi za watalii zikiwasili katika bandari ya Mombasa.

Hii ni baada ya kuwasili kwa meli ya kifahari ya Mv Nautica kutoka Norway ikiwa na  zaidi ya watalii 900.

Meli ya Nautica ni ya nne kutia nang’a bandarini humo katika kipindi cha miezi minne iliyopita.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika halimashauri ya bandari, Haji Masemo amesema kuimarika kwa usalama nchini wakati na baada ya uchaguzi ndio sababu kuu ya kuimarika kwa sekta ya utalii.

“Utalii utazidi kuimarika kote nchini na taifa litasonga mbele bila wasiwasi," alisema Hajj.

Amewataka washikadau wa utalii kuzidi kuboresha na kuimarisha sekta hiyo maradufu ili watalii wa kimataifa waweze kuwasili kwa wingi nchini.

“Tiweze kuwa mstari wa mbele kuboresha utalii wetu,ndio vijana wetu wapate ajira”,alisema Hajj.

Wakati huo huo halmashauri ya bandari nchini imeahidi kumalizika jengo maalum la kuwapokea watalii wanapowasili bandarini humo kabla ya msimu  ujao wa utalii ambao huanza mwezi Septemba.

Sekta ya utalii katika ukanda wa Pwani na taifa kwa jumla ilikumbwa na changamoto ya kudorora kutokana na mashambulizi ya kigaidi yaliyokuwa yakishuhudiwa katika baadhi ya maneneo humu nchini.