Meneja wa shirika la maendeleo la wanawake la Kenya Women ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni tatu, kwa madai ya kutekeleza kosa la wizi wa shilingi milioni 14.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mahakama ilielezwa siku ya Jumatatu kuwa mshtakiwa, Silas Njeru, meneja wa shirika hilo tawi la Mombasa, pamoja na Jacob Kemboi, wanadaiwa kuiba pesa hizo ambazo zilikua mali ya shirika hilo, kati ya tarehe Disemba 18, 2015 na 19, 2015.

Wote walikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkuu Susan Shitub.

Kesi hiyo itatajwa Machi 31, 2016.