Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam Sharaff, amemtaka Ali Kiba kuomba Wakenya msamaha.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Haya yanajiri baada ya Ali Kiba kudai kuwa Sallam alihusika katika kumzimia kipaza sauti alipokuwa anatumbuiza katika Tamasha la Mombasa Rocks lilofanyika wikendi iliyopita.

Kwenye mahojiano na Willy M Tuva, katika kipindi cha Mambo Mseto, Sallam alisema kuwa alihudhuria tamasha hilo ili kujifunza kutoka wasanii wengine na pia kwa kuwa ana uhusiano wa kikazi na Sande, meneja wa Wizkid, ambaye pia ni meneja wa Diamond eneo la Africa magharibi.

Aidha, Sallam amesema kuwa alikuwa tayari ashaondoka katika jukwaa kipaza sauti kilipozimwa, na alikuwa takriban mita 50 kutoka jukwaani wakati wa tukio hilo.

Sallam amemtaka Kiba kuwaomba Wakenya msamaha kwa kutoa ripoti zisizo za kweli, pamoja na kupunguza chuki na Diamond.

Sallam alisema kuwa Ali Kiba alikataa kupanda jukwaani kabla ya Wizkid kinyume na ratiba, na hivyo kupelekea kuvurugika kwa ratiba ya tamasha hilo.

Hatua hiyo inaripotiwa kuwa sababu ya tambuizo la Ali Kiba kukatizwa, ili kumpa Chris Brown, msanii tajika kutoka Marekani, nafasi ya kuwatumbuiza mashabiki wake.

Ali Kiba alitumbuiza nyimbo mbili pekee kabla ya kukatishwa na kumpisha Chris Brown.

Sallam alimalizia kwa kumtaka Kiba kushirikiana vyema na wasanii wenza, ili kukuza muziki wa Africa Mashariki.