Mfanyibaishara mmoja jijini Mombasa ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni tano kwa kosa la kuingiza bidha bandia nchini.
Mshukiwa, Seruwagi Bashir, anadaiwa kuingiza katoni 148 zilizokuwa na vipande 639,360 za kalamu aina ya penseli, zenye thamani ya shilingi 28,771,200 kutoka nchini Ujerumani kupitia Bandari ya Mombasa.
Bashir alikanusha madai hayo siku ya Jumanne mbele ya Hakimu Susan Shitub.
Mahakama ilimuagiza Bashir kulipa shilingi milioni moja pesa taslimu iwapo atashindwa kulipa dhamana hiyo ya shilingi milioni tano.