Mfanyibiashara mmoja katika Kaunti ya Mombasa ameishtaka Benki Kuu ya Kenya na Benki ya Imperial kwa madai ya kutomlipa pesa zake kabla ya benki hiyo kuwekwa chini ya urasimu.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mlalamishi huyo, Ashok Doshi, alisema kuwa hajalipwa pesa zake shilingi bilioni moja miezi sita baada ya benki hiyo ya Imperial kuwekwa chini ya urasimu.

Kupitia kwa wakili wake Francis Kadima, mlalamishi huyo ameitaka Benki Kuu ya Kenya kufuata sheria na kumlipa pesa zote chini ya miezi sita.

Aidha, Bwana Doshi alikashfu hatua ya Benki Kuu kuagizia alipwe shilingi milioni moja kwa kila mwezi, kwa kusema hiyo ni dhuluma kwa wateja wa benki hiyo.

Bwana Kadima alisema kuwa hali hiyo imesababisha mteja wake kungojeka maradhi tofauti pamoja na kuathiri biashara yake.