Mfanyibiashara mmoja wa Mombasa alipigwa risasi na kuuwawa na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake usiku wa kuamkia Jumamosi karibu na eneo la Nyali Cinemax.
Mfanyibiashara huyo alivamiwa na watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki nje ya lango la nyumba yake mwendo wa saa tatu usiku.
Majambazi walimpiga risasi pasi kutoweka ama kuiba mali yoyote ya mwendazake.
Mwendazake aliaga dunia njiani akikmbizwa hospitalini.
Akithibitisha kisa hicho naibu OCPD wa Kisauni Walter Abondo amesema tayari wameanzisha uchunguzi kubaini waliohusika na mauaji hayo.
“Marehemu alipigwa risasi mlangoni kwake wakati alipokuwa ametoka kazini. Jamaa hao hawakuiba chochote kutoka kwa marehemu,” alisema Bw Abondo.