Polisi mjini Naivasha wamemtia nguvuni mfanyibiashara mmoja mashuhuri anayehusishwa na visa vya wizi vinavyolenga bidhaa zinazosafirishwa kwenye barabara kuu ya Naivasha kuelekea Mai Mahiu.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mshukiwa huyo amenaswa hii leo katika duka lake la mbao lililoko eneo la Kayole kwenye barabara kuu ya Nairobi kuelekea Nakuru baada ya mbao zinazoaminika kuibwa kupatikana eneo hilo lake.

Mfanyibiashara huyo anahusishwa na wizi wa mbao zenye dhamani ya shilingi nusu milioni mwezi jana na amekuwa akisakwa kwa muda sasa na vitengo vya usalama.

Kwingineko mwanamme mmoja mwenye umri wa makamo amejitoa uhai baada ya kukosana na mkewe eneo la Ciondo huko Tulaga eneo bunge la Kinangop.

Afisaa mmoja wa polisi wa ngazi ya juu na ambaye hakutaka kutajwa jina lake amedhibitisha tukio hilo na kusema kuwa mshukiwa huyo amepelekwa katika kituo cha polisi cha Nakuru ambako kesi hiyo ilikuwa imeripotiwa.