Jengo la Mahakama ya Mombasa. [barakafm.org]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mfanyikazi wa kituo cha radio cha Sheikh Fm amestakiwa kwa kosa la wizi wa pesa za kituo hicho.

Genoveva Mwongoli Kioko anadaiwa kuiba shilingi 91,980 kati ya Agosti 1,2018 hadi Januari 25,2018 katika afisi za Sheik Fm eneo la Tononoka.

Mwangoli amekanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu Christine Ogweno siku ya Jumatatu.

Mahakama imemuachiliwa kwa dhamana ya shilingi 200,000 ama pesa taslimu ya shilingi 100,000.Kesi yake itasikilizwa februari 7,2018.