Jengo la mahakama ya Mombasa. Mfanykazi wa KPLC amefikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa kwa madai ya kupokea rushwa. [Picha/ the-star.co.ke]
Mfanyikazi mmoja wa shirika la usambazaji umeme la Kenya Power amefikishwa katika Mahakama ya Mombasa na kushtakiwa kwa makosa matatu ya kupokea hongo.Maingi Matheka Mbatha anadaiwa kupokea shilingi elfu tatu kutoka kwa Abdulrahim Maro kwa lengo la kumrudishia umeme uliokuwa umekatwa mnamo Septemba 20, mwaka huu.Maingi amekanusha mashtaka yote matatu mbele ya Hakimu Henry Nyakweba.Mahakama imemuachilia kwa dhamana ya shilingi laki tatu ama dhamana ya shilingi laki moja pesa taslimu.Kesi hiyo itasikizwa Februari 1, mwaka ujao.