Mgororo kati ya Serikali ya Kaunti ya Mombasa na Shirika la huduma kwa vijana NYS, kuhusu ukarabati wa soko la nyama la Marikiti al maarufu Mackinon hatimaye umetatuliwa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hii ni baada ya serikali ya kaunti kutishia kusimamisha ukarabati wa soko hilo, kwa madai ya kutohusishwa katika mipangilio ya ukarabati huo.

Akihutubia wanahabari baada ya mzozo huo kutatuliwa, mwenyekiti wa soko hilo Mushe Mulu, alisema kuwa serikali ya kaunti na ile ya kitaifa zimekubaliana ukarabati wa soko hilo utaendelezwa na Shirika la NYS.

“Hii ni furaha sana kwetu kwa sababu soko hili halijafanyiwa ukarabati kwa muda,” alisema Mulu.

Mulu aliiomba serikali ya kaunti kuwatafutia wafanyabiashara wanaohudumu katika soko hilo mahali pa kuendesha biashara yao soko hilo litakapokuwa likikarabatiwa.

“Itakuwa bora iwapo tutapewa sehemu mbadala ya kuendeleza biashara yetu tukisubiri kukamilika kwa soko hili,” alisema Mulu.