Mgombea wa kiti cha useneta Kaunti ya Mombasa Abdulsalaam Kassim akiwahutubia wanahabari hapo awali [Picha: Hussein Julo/ hivisasa]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mgombea wa kiti cha useneta kupitia chama cha Jubilee Abdulsalaam Kassim amepuzilia mbali madai kwamba kuna njama ya kumpokonya tiketi yake.Kassim alikanusha madai kuwa chama cha Jubilee kinapanga kupatia Naibu Gavana wa Mombasa Hazel Katana tiketi hiyo.Akizungumza mjini Mombasa siku ya Alhamisi Kassim alisema kuwa ripoti hizo ni porojo tu kwa kuwa hakuna njama yoyote inayopangwa na Jubilee.Alisema kuwa porojo hizo zinaenezwa ili kuwapotosha wakaazi wa Mombasa kwa misingi ya kisiasa. Kassim alisisitiza kuwa kura za mchujo za chama cha Jubilee zilitekelezwa katika njia ya huru na haki bila kushuhudiwa kwa visa vyovyote vya udanganyifu.“Ningependa kuwahimiza wanaoeneza uvumi huo kukoma mara moja kwani huenda wakazua taharuki miongoni mwa wakaazi,” alisema Kassim.Hata hivyo, amewahimiza wafuasi wake kutokuwa na hofu yoyote na kujitenga na watu wenye porojo za kuwachanganya kisiasa.Kassim alipata kura 10,785 huku mpinzani wake wa karibu Katana akijizolea kura 9,924 kwenye kura za mchujo zilizofanywa tarehe Aprili 21.