Mwakilishi wa Wadi ya Kongowea Jabez Oduor akiwa kizimbani. [Picha: Osman Suleiman/ hivisasa.com]

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwaniaji wa kiti cha useneta Kaunti ya Mombasa Jabez Odour amefikishwa mbele ya mahakama kwa shutuma za kuzua fujo wakati wa kura za mchujo za chama cha Wiper katika Shule ya msingi ya Fahari huko Nyali siku ya Jumanne.

Jabez, ambaye ni mwakilishi wa wadi ya Kongowea aidha alikabiliwa na shtaka la pili la kuzuia polisi kutekeleza majukumu yao kikatiba.Hata hivyo, Jabez alikanusha madai hayo mbele ya Hakimu Henry Nyakweba siku ya Jumatano.Hakimu Nyakweba alimuachilia mwakilishi huyo kwa dhamana ya shilingi laki moja ama shilingi elfu 50 pesa taslimu.Kesi hiyo itatajwa Mei 8 mwaka huu.