Mgombea wa kiti cha useneta Mombasa Hamisi Mwaguya akiwa na Gavana Hassan Joho katika hafla ya awali. [Picha/ thecoastcounties.com]
Mwaniaji wa kiti cha useneta Kaunti ya Mombasa Hamisi Mwaguya ametangaza kukihama chama cha ODM.Mwaguya ameamua kuwa mgombea binafsi baada ya kushindwa katika kura za mchujo, alizodai kuwa hazikua za haki na huru.“Uchaguzi wa mchujo haukuwa wa huru na haki kwa vile kulikua na wizi wa kura,” alisema Mwaguya.Aidha, alisema kuwa aliamua kuwa mgombea binafsi baada ya kushauriana na wafuasi wake pamoja na watu wake wa karibu.“Nilishauriana na wafuasi wangu na watu wangu wa karibu na wote wakakubaliana niwe mgombea huru,” alisema Mwaguya.Mwaguya hata hivyo alidinda kuzungumzia swala la kuunga mkono mgombea yeyote wa ugavana katika Kaunti ya Mombasa, na kusema kuwa atampigia debe mgombea wa urais wa muungano wa NASA Raila Odinga.Mwaguya alishindwa na wakili Mohammed Faki kwenye uchaguzi wa mchujo wa ODM.