Share news tips with us here at Hivisasa

Madaktari kaunti ya Nakuru wamefutilia mbali mgomo wao kufuatia kubuniwa kwa mkataba wa kuwawezesha kurejea kazini.

Mkataba huo umetiwa saini na wawakilishi wa kaunti ya Nakuru pamoja na viongozi wa muungano wa madaktari Ijumaa ya tarehe 18 Desemba.

Madaktari hao walirejea kazini jana Ijumaa huku serikali ya kaunti ya Nakuru ikubali kushughulikia matakwa yao.

Hii ni baada ya madaktari 96 kuanza mgomo baridi kuanzia Jumatano ya tarehe 9 Desemba kutokana na kucheleweshwa kwa hatua ya kuwapandisha vyeo na pia kucheleweshwa kwa marupurupu yao kwa muda wa m,iaka miwili iliyopita.

Uchunguzi uliofamnywa na wanahabari wa Nakuru jana Ijumaa katika hospitali kuu ya mkoa wa bonde la ufa iliyo Nakuru ulionyesha kuwa wahudumu wa afya walianza kuwahudumiwa wagonjwa huku wengine wakilazwa katika wadi mbalimbali.

Mwenyekiti wa muungano wa kutetea madaktari wa Kenya Medical Practitioners And Dentists Union (KMPDU) kanda ya kusini mwa bonde la ufa Austion Oywer alikuwa amesema hapo awali kuwa iwapo kaunti ya Nakuru haingetekeleza matakwa yao kufikia hapo jana Ijumaa, wangelemaza shughuli zote za kimatibab katika vituo vyote vya kiafya vya serikali kwa kufanya mgomo.

Muungano huo katika muda wa mwaka mmoja uliopita umekuwa ukipigania jhatua ya madkatari waliostaafu kupandishwa vyeo, huku ikiarifiwa kuwa hatua hiyo haijakuwa ikifua dafu licha ya majadiliano mbalimbali ambayo yamekuwa yakifanywa tanhu mwezi Juni katika ya serikali na wahudumu wa afya.

Hata hivyo, mkataba huo uliotiwa saini na viongozi wa KMPDU wakiongozwa Oywer na afisa mkuu wa afaya ya uma kwenye kaunti ya Nakuru Daktari Samwel Mwaura uliafikia kuwa madaktari wote walioafikiwa vigezo vye kupandishwa vyeo watapandishwa vyeo na kwamba watapokea marupurupu hayo kufikia Januari tarehe 31 mwaka ujao 2016.