Mgomo was madaktari na wauguzi jimbo la Nakuru umesitishwa na korti ya wafanyikazi ili maafikiano kati ya serikali ya kaunti na madaktari pamoja na wauguzi ifikiwe.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mgomo huu umesabashisha ma mia ya wagonjwa kutohudumiwa katika hospitali kuu ya Rift Valley, huku zaidi ya wafanyi kazi 2,402 katika sekta ya afya wakishiriki katika mgomo huu.

Sehemu ambazo zimeathirika ni pamoja na Gilgil, Naivasha, Rongai na Molo.

"Serikali ya kaunti haijatulipa marupurupu yetu na wafanyikazi wengi wamesalia katika vyeo walivyopewa wakati walipoajiriwa," alisema mmoja wao ambaye hakutaka kutajwa jina.

Wafanyikazi hawa wanadai kwamba serikali ya kaunti imekataa kusikiza malalamishi yao.