Mhudumu mmoja wa klabu ya Radinas ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Godwin Muteshi, alifariki alipokuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Nyali iliyoko Likoni.

Inaripotiwa kuwa marehemu alikuwa kazini wakati wa tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia siku ya Jumamosi.

Akithibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi eneo la Likoni Willy Simba alisema kuwa majambazi hao walitoroka kwa miguu baada ya kutekeleza uhalifu huo.

"Polisi walipata maganda mawili ya risasi aina ya G3. Tayari tumeanzisha msako mkali ili kuwanasa majambazi hao ambao wanatuhumiwa kuwahangaisha wakaazi wa Likoni,” alisema Simba.