Mhudumu wa duka la M-Pesa amefikishwa mahakamani kujibu shtaka la kumuibia mwajiri wake zaidi ya shilingi laki moja.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Jumatano kuwa mshtakiwa, Noleen Munguti, anadaiwa kumuibia mwajiri wake Agnes Mueni, Sh123,036 mnamo Mei 17, 2016 katika eneo la Guraya.

Mshtakiwa huyo alikubali shtaka hilo mbele ya Hakimu Teresia Matheka, na kuomba mahakama kutomhukumu kifungo cha jela.

Bi Munguti aliitaka mahakama kumpa muda wa kuzilipa pesa hizo.

Hakimu Matheka aliagiza afisa wa kifungo cha nje kutoa ripoti kuhusu mshtakiwa huyo tarehe 28 mwezi May, kabla ya mahakama kutoa hukumu yake.