Chuo kikuu cha moi kiliandaa sherehe za kufana katika awamu ya pili ya kuhitimu kwa zaidi ya maafala 2000.
Sherehe hizo ambazo ni za mara ya thelathini na moja, tangu kuanzishwa kwa chuo hicho ziliongozwa na chansela wa chuo hicho, Profesa Miriam were.
Aidha Wahitimu walituzwa na shahada na stashahada katika taalamu mbalimbali naye chansela huyo.
Katika hotuba yake naibu chansela Profesa Richard Mibey alisema kuwa chuo kikuu cha Moi kinatajika katika sekta mbalimbali huku ikijivunia kampuni yake ya Rivatex, inayowapa mafunzo wanafunzi hasa wale wa taaluma ya uhandisi.
Aidha Mibey aliwapongeza maafala kwa kuhitimu katika vitivo mbalimbali na akawapa changamoto kuwajibika katika ulimwengu wa ajira, huku akiwataka waangazie kujitengea nafasi za ajira badala ya kusuburi kuajiriwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chuo hicho, Profesa Jenesio Kinyamario alidokeza kuwa chuo kikuu cha Moi kinakabiliwa na changamoto cha mabweni lakini akasema kuwa tayari mikakati imewekwa ili kushirikiana na washikadau wa kibinafsi katika ujenzi wa mabweni mapya.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Michael Kahiti aliyewakilisha waziri wa elimu, Fred Matiang'i. Katika ujumbe wa waziri matiang'i na ulisomwa naye Kahiti, chuo kikuu cha Moi kimepiga hatua kubwa katika kuimarisha usalama.
''Usalama umeimarishwa, maafisa wa usalama wanapiga kambi kila siku, hakuna hofu yeyote katika chuo hiki. Aidha Matiang'i alitoa wito kwa vyuo vikuu kote nchini kujihusisha na maendeleo ya taifa kupitia kwa masomo.