Aliyekuwa afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya mawasiliano Safaricom Michael Joseph, anatarajiwa kupokezwa rasmi wadhfa wa chancellor wa chuo kikuu cha Maseno siku ya Jumatano, wakati wa sherehe za 14 za kufuzu kwa mahafala chuoni humo.
BwJoseph aliteuliwa chancellor wa chuo kikuu cha hicho na rais Uhuru Kenyatta mapema mwaka huu, na atachukua nafasi ya Prof Florida Karani ambaye amekuwa kwenye wadhifa huo kwa kipindi cha miaka sita.
Kwa mujibu wa ujumbe uliotumwa kwa vyombo vya habari na mkurugenzi wa mawasiliano ya umma katika chuo hicho Japher Otieno, Michael Joseph atakuwa Chancellor wa nne katika historia ya chuo hicho.
Waziri wa elimu Prof Jacob Kaimenyi, ni miongoni mwa viongozi na wadau wa elimu wanaotarajiwa kuhudhuria sherehe za hizo.
Joseph alikuwa afisa mkuu mtendaji wa Safaricom kwa miaka 11, kati ya mwezi Juni mwaka 2000 na Mwezi Juni mwaka 2011.
Chini ya uongozi wake, Kampuni ya Safaricom ilipata wateja wengi ambao inajivunia kwa sasa.
Huenda chuo kikuu cha Maseno, kikaimarika zaidi chini ya uongozi wake.