Serikali ya kaunti ya Nakuru imetenga zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano kutumika katika shughuli ya upanzi wa miti msimu huu wa mvua
Afisa mkuu katika wizara ya mazingira Nelson Maara Tanui amesema kuwa pesa hizo zitatumika katika kupanda miche zaidi ya elfu mia moja katika kila eneo bunge.
Akiongea jumatatu katika wadi ya soali wakati wa shuguli ya kuzindua kampeni hiyo,Tanui alisema kuwa serikali ya kaunti itawahusisha wasimamizi wa makanisa na shule katika kufanikisha hilo.
“Nakuru ni kaunti ambayo tumezungukwa na misitu na ni wajibu wetu kulinda hii misitu kwa kupanda miti zaidi na musimu huu wa mvua tumetenga silingi milioni ishirini na tano kutumika katika kupanda miche zaidi,” alisema Tanui.
Aliongeza “tutahusisha wanafunzi na wanavijiji ili kuhakikisha kuwa tunapanda miti mingi zaidi tuwezavyo kabla ya mvua kukatika na tutapanda miche elfu mia moja katika kila eneo bunge,”.
Mwanamazingira kutoka Rongai Mary Waikite alisifu hatua hiyo na kusema kuwa itasaidia pakubwa katika kulinda misitu ya kaunti na kuhifadhi mazingira.
“Hii ni hatua ambayo inafaa kuungwa mkono na kila mpenda mazingira kwa kuwa itafaidi hata vizazi vijavyo katika eneo hili letu,” alisema.