Mbunge wa Likoni Mishi Mboko.[Osman Suleiman]

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mbunge wa Likoni Mishi Mboko ametoa ushahidi wake kwa mara ya kwanza katika mahakama kuu ya Mombasa kwenye kesi ya kupinga ushindi wake wa uchaguzi wa Agosti nane.

Kesi ya kupinga ushindi wa Mboko iliwasilishwa mahakamani na aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Masoud Mwahima ambaye aliwania kupitia chama cha Jubilee.

Akitoa ushahidi huo siku ya Jumatatu mbele ya jaji Erick Ogola wa mahakama ya Mombasa,Mishi alipinga madai kuwa kulikuwa na wizi wa kura katika vituo vya kupigia kura eneo bunge la Likoni.

Aliongeza kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa uwazi na haki na kuongeza kuwa watu wa Likoni walimchagua kwa moyo mmoja kinyume na inavyodaiwa na Mwahima.

Aidha,amepinga kuwa aliwashurutisha wasimamizi wa uchaguzi eneo bunge la Likoni ili kumtangaza mshindi kwenye uchaguzi huo kama  inavyodaiwa na Mwahima.

Mishi alisema kuwa hana ufahamu kama nguvu za umeme zilipotea wakati wa kuhesabiwa kwa kura hizo katika kituo kikuu cha kuhesabiwa kura cha Likoni school for the blind kama anavyodai Mwahima.

Ameongeza kuwa hana ufahamu wowote wa iwapo mawakala wake walishikwa na kufikishwa polisi kwa madai ya kuhusika na wizi wa kura.

Wakati huo huo amesema kuwa hana ufahamu iwapo watu walisafirishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine ili kupiga kura katika vituo vya eneo bunge la Likoni.

Miezi miwili iyopita mbunge za zamani Masoud Mwahima aliambia mahakama kuwa hakukuwa na umeme katika kituo kikuu cha kujumuisha kura cha Likoni School for the blind.

“Hakukuwa na umeme na iliwalazimu maafisa wa IEBC kutumia mwangaza wa simu kujumuisha kura hizo. Ni wazi kuwa kulishuhudiwa wizi wa kura,” alisema Mwahima.

Mwahima alidai kuwa mawakala waliohusika katika uchaguzi huo wa ubunge eneo la Likoni walikuwa bandia na wala sio wa chama cha Jubilee.

“Mawakala waliotumika kusimamia kura hawakuwa wa Jubilee wala siwajui kamwe. Hao ni mawakala bandia na walifanywa kuokotwa mitaani,” alisema Mwahima.

Mwahima alidai kuwa mawakala waliohusika katika uchaguzi huo wa ubunge eneo la Likoni walikuwa bandia na wala sio wa chama cha Jubilee.

“Mawakala waliotumika kusimamia kura hawakuwa wa Jubilee wala siwajui kamwe. Hao ni mawakala bandia na walifanywa kuokotwa mitaani,” alisema Mwahima.