Misongomano ya watu na magari imeendelea kushuhudiwa Nakuru mjini siku moja tu kabla ya Krisimasi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwandishi huyu alipozuru mjini masaa ya asubuhi tarehe ishirini na nne, aliweza kukumbana na misongomano katika maeneo mbalimbali.

Steji za kuegeshea magari zimezidi kuvutia watu wengi hasa wanaotarajia kusafiri kuelekea sehemu tofauti hapa nchini. Hata magari yanayotumikia wakaaji wa vitongonji vya mji yaliweza kuwa na watu wengi. Kwa bahati nzuri, imeibuka kwamba wahudumu wengi wa magari ya uchuuzi hawajaongeza nauli kama ilivyo kawaida.

Katika magari ya Crossroad Travellers yanayobebea katika kituo cha kuuzia mafuta cha Shell, nauli ya kusafiri hadi Nairobi ilikuwa imeshuka hadi shilingi mia mbili.

“Kwangu hii ni sikukuu Mungu aliyoituma,” mjeja mmoja alisikika akidai huku akiriabiri gari.

Vilevile, misongomano ilishuhudiwa katika maduka ya jumla kama vile Tuskys, Ukwala, Nakumatt na mengine. Sehemu zinazofutia watu wengi ndani ya maduka haya ni sehemu za chakula, manguo na elektroniki.

Wengine ambao wamekuwa na wingi wa wateja ni wachuuzi wa manguo mitaani. Mwandishi alipoongea na Samuel Maina ambaye anauza manguo ya mtumba kando ya supermarket ya Stagematt Chapchap, Samuel alikuwa na haya ya kusema,

“Yenyewe krismasi hii nimeonekaniwa. Kwa wiki moja iliyopita, nimeweza kuuza zaidi ya nilivyouza katika mwezi mzima wa Novemba,” alisema Maina huku akiendelea kuhudumia wateja wanaomiminika kuchagua nguo zake.

Wanaopeana huduma za kutuma na kupokea pesa waliweza kuwa na biashara iliyonoga msimu huu. Janet Akinyi ambaye ameajiriwa katika duka la M-Pesa anasema wajeja wameongezeka sana wakati huu.

“Inaonekana watu wengi wanaona ni heri kuwatumia wapendwa wao pesa za matumizi baabala ya kusafiri. Wanaoweka na kutoa pesa ni wengi na nimekuwa busy tangu nifungue mwendo wa saa moja na nusu. Hata mimi mwenyewe sisafiri na imenibidi niwatumie wazazi wangu pesa za krismasi,” anasema Janet.

Maeneo mengine inayoshuhudia misongamano ni mahoteli, soko ya vyakula, na sehemu zingine za burudani.