Gavana wa Kwale Salim Mvurya katika hafla ya awali. [Picha/ nation.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Mkaazi mmoja wa Kaunti ya Kwale amewasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wa Gavana Salim Mvurya.Mwamlole Tchapu M’bwana alifika katika Mahakamani ya Mombasa siku ya Jumatano akiwa ameandamana na mgombea mwenza wa Chirau Ali Mwakwere, Mwandogo Omar Chigodi.Akizungumza nje ya jengo la Mahakama ya Mombasa, Chigodi alisema kuwa uchaguzi wa Kwale ulikumbwa na udanganyifu mkubwa na kutaka ushindi wa Mvurya kufutiliwa mbali.“Kumekuwa na wizi mkubwa wa kura na hatutakubali ushindi wa Mvurya kabisa,” alisema Chigodi.Mvurya aliibuka mshindi katika uchaguzi wa August 8 kwa kura 119,914, huku Mwakwere akipata kura 29, 491.Issah Kipera alikuwa wa tatu na kura 28,713 huku akifuatwa na Sammy Ruwa na James Dena waliopata kura 4,996 na 1,460 mtawalia.