Idara ya polisi pamoja na afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma zimemhusisha Haniya Saggar, mke wa marehemu Sheikh Aboud Rogo na mitandao ya kigaidi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza katika mahakama ya Shanzu, mwendesha mashtaka Daniel Wamotsa kutoka afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma nchini allisema kuwa madai yanayomkabili mshukiwa huyo yanahatarisha usalama wa taifa.

“Mshukiwa huyu anajihusisha na mitandao hatari ya kigaidi duniani,” alisema Wamotsa.

Siku ya Jumanne, Wamtosa alisema kuwa mshukiwa huyo anadaiwa kushirikiana na mitandao ya kigadi nchini Iraq na Syria.

“Idara ya upelelezi inajitahidi kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na madai hayo,” alisema Wamotsa.

Wakili wa Saggar Mbugua Murethi alipinga madai hayao na kusema hiyo ni njama ya kukandamiza haki za mteja wake, kwa kuwa hana ufahamu wowote kuhusiana na mitandao ya kigaidi.

Haniya Sagar, Nastaheno Ali Thalili, Luul Ali Thahil na Zamzam Abdi Abdallah wanadaiwa kukosa kutoa habari kwa polisi kuhusu uvamizi wa Kituo cha polisi cha Central.

Mahakama ya Shanzu itaotoa uamuzi wa dhamana siku ya Alhamisi.