Wafuasi wa MRC.[intelligencebriefs.com]
Kauli hii imetolewa na mmoja wa mkereketwa wa kisiasa eneo bunge la Malind Jamal Shehe,ambaye amesema iwapo viongozi hao watashirikiana basi Pwani itaweza kujitenga bila mvutano wowote.
Ameutaja ubabe wa kisiasa unaoshuhudiwa kati ya chama cha Jubilee na mrengo wa Nasa, utafikia kikomo endapo azma ya wapwani kujitenga itatimia.
“Mvutano wa Jubilee na Nasa itafika mwisho pale Pwani itajitenga, itakuwa tunajimiliki wenyewe pasi kushirikisha watu wengine”,alisema Shehe.
Akizungumza na wanahabari,siku ya Ijumaa,Shehe alisema kuwa kwa muda mrefu eneo la Pwani limetengwa katika nafasi kuu serikalini,huku vijana wengi eneo la Pwani hawama ajira.
“Pwani imetengwa kwa muda sasa,vijana hawana ajira wanaangaika kutafuta ajira tangu taifa lipate madaraka”,alisema Shehe.
Amelitaja eneo la Pwani kama lenye rasilimali nyingi ambazo,ndio tegemeo kuu kwa wakazi wa Pwani na iwapo litajitenga rasilimali hizo zinatosha kukidhi mahitaji ya wapwani.
“Tuko na rasilimali nyingi ambazo zikitumiwa vyema zinatosha kukidhi mahitaji ya wapwani wote”,alisema Shehe.
Wakati huo huo, Shehe amewakosoa viongozi wakuu wa mabaraza ya dini ya Kiislamu kwa kuwataja kama wanaoegemea mrengo mmoja wa kisiasa.
Amewataja viongozi hao kuwa wenye ubinafsi na kwamba utendakazi wao umekuwa wa kutenganisha jamii ya Waislamu kwani wamekosa kuwatetea Wapwani kama jamii moja.
Kadhalika amesema viongozi hao hawatambuliki kwani hawajachaguliwa na jamii ya Waislamu kuwawakilisha kama wasemaji wao.