Mkurugenzi mpya wa bodi ya maji eneo la Pwani Jacob Kimutai akiwahutubia wanahabari hapo awali. [Photo/ the-star.co.ke]
Mkurugenzi mpya wa bodi ya maji eneo la Pwani Jacob Kimutai ameagizwa kufika mbele ya Mahakama ya Viwanda jijini Mombasa.
Kimutai ametakiwa kuweka wazi kwa nini alianza kazi licha ya kuweko agizo la Mahakama la kusitisha uteuzi wake.Kimutai alichukua nafasi ya Joseph Omwange ambaye alihudumu kama kaimu mkurugenzi wa bodi hiyo kwa muda wa miezi 17.Hatua hii inajiri baada ya Tume ya kutetea haki za binadamu ya Commission for Human Rights and Justice kutaka mkurugenzi huyo kufungwa miezi sita jela kwa ukiukaji wa agizo la mahakama.Aidha, tume hiyo imetaka mahakama kumzuia Kimutai kuhudumu katika wadhfa huo.Kuteuliwa kwa Kimutai kulisababisha kusitishwa kwa huduma za usambazaji wa maji katika kaunti zote sita za Pwani.Kesi hiyo itasikizwa Mei 28 mwaka huu mbele ya Jaji Onesmus Makau.