katika michezo siku za awali ili kuongoza kamati za michezo.
Haya yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa elimu katika kaunti ya Kisii Richard Chepkawai.
Jamii ya Wakisii ilikuwa ya kwanza kutoa mwanariadha kutoka Afrika kushinda medali ya dhahabu kupitia kwa mkongwe wa riadha Nyantika Mayioro katika miaka ya sitini, lakini ukosefu wa wanariadha wa sampuli yake umesababisha mchezo huo wa riadha kufifia katika kaunti za Kisii na Nyamira.
Hata hivyo, Chepkawai bado ana matumaini kuwa Kisii itainuka tena katika riadha, huku akishauri viongozi kutoka Kaunti ya Kisii kuwatambua wanariadha wa zamani na wa sasa ili kuwapa nafasi kwenye michezo hiyo katika kukuza talanta miongoni mwa vijana wa kaunti hiyo.
Bwana Chepkawai alikuwa akiongea siku ya Ijumaa jioni katika ofisi yake, ambako alipongeza baadhi ya shule katika kaunti hiyo ambazo zimeanza kuboresha viwango vya riadha, mojawapo ikiwa Shule ya Mseto ya Nyota, ambayo imekuwa ikitamba katika mbio fupi kwa miaka mitatu sasa, na akashauri walimu wakuu wa shule nyingine kuiga mfano wa shule hiyo kwa kukuza vipawa vya wanafunzi.
“Kisii sasa imeanza kuinuka, na nawaomba viongozi wote kukumbatia vipawa vya watoto wetu na vilevile tutambue wanariadha wa zamani kama Mayioro (Nyantika), unaona wanajamii wa Kalenjin vile wamemtambua Kipchoge, nasi tuige mfano huo, Kip-Keino sasa anakaa kama mfalme,” Chepkawai alitoa changamoto.