Mkurugenzi wa huduma za matibabu katika Kaunti ya Nyamira Jack Magara amejitokeza kuwapongeza wakazi wa kaunti hiyo kwa kushirikiana na maafisa waliokuwa wakiwapa watoto chanjo dhidi ya ugonjwa wakupooza almaarufu polio. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubia wanahabari mjini Nyamira siku ya Ijumaa, Magara alisema kuwa utafiti umebaini kuwa idadi kubwa ya wakazi wa kaunti hiyo walishirikiana kiukamilifu na maafisa waliokuwa wakiwapa watoto chanjo kwa siku tano, akihoji kuwa idadi ya watoto waliochanjwa ilipita kiwango cha asilimia 100%. 

"Tulikuwa tunatarajia kuwachanja watoto 127,147, lakini idadi hiyo ikafikia watoto 129,991 ambayo ni asilimia 102%, asilimia iliyo afikiwa kwanzia tarehe 5- 9 mwezi huu wa desemba," alisema Magara. 

Magara aidha aliwapongeza wazazi waliojitokeza kuhakikisha kuwa wanao wamepokea chanjo bila ya kushawishika na dhana kuwa chanjo hiyo ilikuwa na madhara yan kiafya. 

"Nawashukuru sana wazazi kwa kwa kuhakikisha kuwa wanao wamepewa chanjo hiyo bila kuzingatia fununu kuwa chanjo hiyo ilikuwa na madhara ya kiafya, hasa kwa kuathiri uzazi na hata pia kusababisha uvimbe wa miguu," aliongezea Magara.