Mkutano wa siku mbili wa mawaziri unaoongozwa na rais Uhuru Kenyatta umeanza katika hoteli ya Great Rift Valley Lodge mjini Naivasha hii leo jumatatu.
Akizungumza kwa dakika chache kabla ya mkutano huo kuanza hii leo asubuhi, Rais Uhuru Kenyatta amekariri kwamba wanaazimia kuhusiana na maswala wanayofaa kuyapa kipaumbele.
Aidha, rais Kenyatta amesema kuwa wanajadili kuhusiana na maswala ambayo wanafaa kuyatekeleza wakizingatia rasilmali zilizopo kwa sasa.
Taarifa iliyotolewa hapo awali na kitengo cha rais cha mawasiliano iliarifu kuwa mkutano huo utajadili na kuklubaliana kuhusiana na maswala yanayofaa kupewa kipaumbele kwenye bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2016/2017 .
Ni mkutano ambao pia umehudhuriwa na naibu rais William Ruto, mawaziri pamoja na makatibu wa kudumu wa wizara mbalimbali.
Mkutano huu unajiri siku chache baada ya mkutano wa mammbi ya kurudisha shukrani kwa kutupilia mbali kwa kesi dhidi ya naibu Rais William Ruto kufanyika kwenye uwanja wa Afraha kwenye kaunti ya Nakuru..
Ni mkutano uliohudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta ,naibu wake William Ruto , viongozi wa kitaifa, wale wa kaunti ya Nakuru pamoja na watu wa tabaka mbalimbali.