Jengo la Mahakama ya Mombasa. [Picha: Haramo Ali/ hivisasa]
Mkwe wa Mwakilishi wa Wanawake Kaunti ya Mombasa Mishi Mboko amefikishwa kizimbani kujibu shtaka la mauaji.
Tariq Twalib anadaiwa kuhusika katika mauaji ya Peter Munyika mnamo Machi 23 katika eneo la Khoja huko Majengo.
Tariq anadaiwa kulipa gege la vijana lilompiga Munyika, ambaye alikua bawabu wa Tariq, kwa madai ya kumuibia shilingi 1,500.
Hata hivyo, Tariq alikanusha mashtaka hayo mbele ya Jaji Dora Chepkwonyi, na kuachiliwa lwa dhamana ya shilingi laki tano.
Tariq ni mume wa Hafidha Wakesho ambaye ni binti wa Mishi Mboko.
Kesi hiyo itasikizwa Juni 21, mwaka huu.