Mlinzi wa Shule ya msingi ya Consolata amehukimiwa miaka 15 gerezani kwa kosa la kufanya mapenzi na mtoto wa miaka 17.
Mahakama ilielezwa kuwa mshukiwa, Mjera Matindi, alitekeleza kitendo hicho katika shule hiyo iliyoko Likoni, mnamo Februari 27, 2016.
Mshtakiwa huyo alikubali shtaka hilo siku ya Jumatatu na kuiambia mahakama kuwa alishiriki kitendo hicho alipompatia hifadhi mtoto huyo alipofukuzwa nyumbani kwao.
Matindi alielezea mahakama kuwa mtoto huyo alifukuzwa baada ya kuchelewa kurudi nyumbani, na kuomba hifadhi kwake.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu katika Mahakama ya Mombasa Henry Nyakweba, alisema kuwa mshtakiwa huyo hafai kutumikia kifungo cha nje na kuamua kumfunga miaka 15 gerezani.
Mjera yuko na siku 14 za kukata rufaa kupinga uamuzi huo.