Gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua amewakashifu baadhi ya wanasiasa kutoka kaunti hiyo kwa kile amedai ni kucheza siasa potovu.
Kinuthia alidai kuna kundi la wanasiasa ambalo lilipanga kumuaibisha mbele ya rais.
Hii ni baada yaya gavana huyo kuzomewa na umati wakati wa ziara ya rais Nakuru mjini.
Akiongea Jumamosi mjini Naivasha, Kinuthia alisema viongozi wanafaa kucheza saiasa komavu.
“Kuna baadhi ya watu ambao wangali wanacheza siasa zilizopitwa na wakati, siasa hizo zimepitwa na wakati,” Kinuthia alisema.
“Walisema mimi ni mbaya, wanipee nafasi nihudumu tutakutana kwa uwanja sisi wote 2017,” Kinuthia alisema.