Mgombea wa kiti cha ubunge Nyali Mohammed Ali katika hafla ya awali. [Picha/ kenya-today.com]
Mgombea huru wa kiti cha ubunge Nyali Mohammed Ali amekashifu uongozi wa Kaunti ya Mombasa.
Akiwahutubia wakaazi katika katika mkutano ulioandaliwa na wagombea huru katika ukumbi wa Frere Town, Ali alidai kuwa kandarasi nyingi za kaunti hupewa kampuni zinazohusishwa na viongozi wakuu wa kaunti, hatua aliyosema inanyanyasa wakaazi.
“Kandarasi zote za kaunti zinatolewa kwa njia ya ubaguzi kwani ni familia kadhaa tu zinazonufaika ilhali vijana wanazidi kuhangaika kufuatia ukosefu wa ajira,” alisema Ali.
Ali amewataka wakaazi wa Mombasa kuwa makini wanapochagua viongozi wa kisiasa ili kuepuka kukandamizwa kimaendeleo.
“Changueni viongozi wenye malengo ya maendeleo na muasi wale wafisadi na wakandamizaji,” alisema Ali.
Aidha, alisema kuwa atamuunga mkono kinara wa NASA Raila Odinga katika kinyanganyiro cha urais lakini katika ngazi za chini wananchi wenyewe ndio watakaoamua viongozi watakaowachagua.
Hata hivyo, Raila ameweka wazi kuwa hataunga mkono mgombea huru yeyeto na kuwataja kama wasiokuwa na malengo.
Aidha, amewataka wafuasi wa Nasa kutounga mkono wagombea huru.