Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa eneo bunge la Rongai Raymond Moi amewaahidi maskota wa Shamba la Banita kwamba mzozo wa muda mrefu wa shamba hilo utasuluhishwa hivi karibini.

Akizungumza katika kikao na wazee kutoka jamii mbili ambazo zimekuwa zikilumbana katika hoteli moja mjini Nakuru siku ya Jumanne, mbunge huyo ambaye pia ni mwanachama wa kamati ya bunge kuhusu ardhi alisema kuwa utata wa ardhi hiyo yenye ekari elfu 14, utatatuliwa hivi karibuni baada ya bunge kurejelea vikao vyake tarehe Februari 9, 2016.

Moi alisema kuwa kufikia sasa, kamati hiyo imekwisha andaa ripoti itakayowasilishwa bungeni kujadiliwa punde tu bunge itakaporejelea vikao vyake.

Mbunge huyo alisema kuwa ameshangazwa na hatua ya baadhi ya watu kutoka maeneo ya mbali kujitokeza wakitaka ardhi hiyo.

Mbuge huyo alisema kuwa kamati hiyo inalenga kutenga asilimia 60 kwa wakaazi wa eneo hilo ambao ni wafugaji, huku asilimia 40 ikiwaendea watu waliokuwa wakifanya kazi katika shamba hilo hapo awali.

Moi alisema kuwa walengwa watapata ekari kumi kila mmoja.

Mwenyekiti wa Tume ya Ardhi katika Kaunti ya Nakuru Frank Kimbelekenya aliunga mkonomatamshi hayo huku akisema kuwa mazungumzo baina ya pande zinazozozana ndiyo suluhu katika mzozo huo wa ardhi.

Mkutano huo uliwaleta pamoja vingozi na wanachama kutoka jamii za eneo hilo wapatao 27 kwa hisani ya shirika la Idpac linalotetea haki za wakimbizi humu nchini.