Serikali ya Kaunti ya Mombasa ikishirikiana na ile ya Uchina imetia saini mkataba wa kuendeleza uhusiano mwema baina ya mji wa Mombasa na mji wa Fuzhou.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mkataba huo unatarajia kuboresha sekta ya biashara, kuimarisha uchumi na miundo msingi, ili kuwawezesha vijana kupata ajira.

Akiongea na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumatatu baada ya kutia saini mkatabha huo, Mwenyekiti wa baraza la mji wa Fuzhou, Yang Yue alisema kuwa ushirikiano huu utawasaidia wakaazi katika kuboresha afya yao, elimu, pamoja na kukarabati mitaro ya maji taka.

"Tunataka kuhakikisha kuwa Kaunti ya Mombasa na mjiwa Fuzhou kule Uchina zinafanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa maswala ya afya, miundo msingi, elimu na maji yanaangaziwa vyema na kuwafaidi wakaazi,” alisema Yue.

Kwa upande wake Naibu Gavana wa Kaunti ya Mombasa Bi Hazel Katana alisema kuwa mkataba huo utasaidia kuboresha mji wa Mombasa.

"Tunaimani kuwa mkataba huu utatusaidia zaidi kama wakaazi wa Mombasa kuboresha uhusiano mwema na wenzetu wa kule Uchina, ili maswala muhimu ya miundo msingi kuimarishwa,” alisema Hazel.