Peterson Maelo ameteuliwa kuwa kamanda mpya wa polisi katika Kaunti ya Mombasa.
Hii ni katika mabadiliko yaliyotangazwa na tume ya kitaifa ya huduma ya polisi mapema siku ya Jumanne.
Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa akihudumu katika nafasi hiyo na kama kamanda wa polisi ukanda wa Pwani Julius Wanjohi ataendelea kusimamia ukanda wa Pwani.
Aliyewahi kuhudumu kama OCPD wa Mombasa Kisiwani Geoffrey Maiyek kwa sasa atahudumu kama OCPD wa Buruburu akichukua nafasi ya Richard Kerich, aliyehamishwa kuwa naibu kamanda wa polisi wa Kaunti ya Nairobi.
OCPD wa Changamwe Joseph Muthee amehamishwa hadi eneo la bonde la ufa katika wadhfa wa afisa mkuu wa trafiki eneo hilo na nafasi yake kuchukuliwa na Stephen Cheteka.
Aliyekuwa afisa mkuu wa upelelezi Kaunti ya Nairobi Nicholas Kamwende ambaye alihamishwa kuwa afisa mkuu wa upelelezi kanda ya Pwani Februari 7 ameitwa katika makao makuu ya polisi jijini Nairobi katika mabadiliko hayo.