Kaunti ya Mombasa ni miongoni mwa Kaunti nne zilizoshiriki katika maonyesho ya kihistoria na utamaduni nchini Ujerumani.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza kwenye mahojiano na mwandishi huyu siku ya Jumatatu mjini Mombasa, Mkuu wa Idara ya utalii katika Kaunti ya Mombasa Binti Omar alisema kuwa maonyesho hayo ni baadhi ya mikakati ya kuboresha sekta ya utalii nchini.

Omar alisema walitumia maonyesho hayo kuwaelimisha watalii kuhusu urithi wa utamaduni wa Kiswahili, pamoja na vyakula vya kitamaduni vinavyopatikana katika Kaunti ya Mombasa.

Omar aidha alichukua fursa hiyo kuwahimiza watali kutoka Ujerumani na nchi zingine za kigeni kuhudhuria maonyesho ya kitamaduni yatakayoandaliwa katika Kaunti ya Mombasa mwezi Agosti.